Advertisement

KOICA CONTRACTS IPOSA KISHAPU PROJECT BUILDING WORTH TSH. 57.9 MILLION



 The Korea International Cooperation Agency (KOICA) has officially handed over the IPOSA project building worth 57,900,000 Shillings to the Executive Director of the Kishapu District Council, Emmanuel Johnson. The building is located in Negezi Village, Ukenyenge Ward, Kishapu District in Shinyanga Region.


The handover took place on March 13, 2026, in a ceremony attended by various government leaders, education stakeholders, and local residents.

Speaking at the event, IPOSA Project Manager, Hyunjoo Song, said they are pleased with the completion of construction and the enrollment of students at the center, explaining that the center would be an important opportunity for young people to gain knowledge and skills to help them achieve economic success in their lives.







          Na Sumai Salum-Kishapu
Meneja wa Mradi wa IPOSA, Hyunjoo Song, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya jengo la mradi wa Iposa lenye thamani ya Tsh. milioni 57.9 unaofadhiliwa na KOICA kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga  Machi 13,2026 ulioko Kijiji cha Negezi Kata ya Ukenyenge wilayani humo


Song amewataka wanafunzi kutumia fursa hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili waweze kuboresha maisha yao na kuchangia maendeleo ya jamii.


“Nipongeze Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hadi kwa watendaji wake katika ngazi ya Halmashauri kwa namna walivyoonesha uwajibikaji katika kusimamia fedha zilizotolewa na kuhakikisha lengo lililokusudiwa linafikiwa. Kituo hiki ni cha kwanza kwa ubora kati ya vituo vyote tulivyotembelea,” amesema Song.


Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kamishina wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST), Felister Mapunda, ameipongeza serikali kupitia wizara hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa kushirikiana katika kupokea na kusimamia mradi huo.


Amesema mradi wa Kishapu umewekwa katika eneo sahihi na kuwataka walimu kuhakikisha wanawapatia wanafunzi ujuzi unaohitajika ili wanapomaliza mafunzo wawe na stadi zitakazowasaidia kujitegemea kimaisha.


“Niwaambie tu kwamba Tanzania ina halmashauri 184 lakini vituo vya aina hii vipo 27 tu. Hivyo Kishapu mmepata nafasi ya kipekee ambayo si ya kawaida. Inaonekana vijana wa hapa wana bidii ndiyo maana mmejitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata ujuzi wa kuendeleza maisha yenu,” amesema Mapunda.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Profesa Philipo Sanga, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya jengo la mradi wa Iposa lenye thamani ya Tsh. milioni 57.9 unaofadhiliwa na KOICA kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga  Machi 13,2026 ulioko Kijiji cha Negezi Kata ya Ukenyenge Wilayani Kishapu mkoani humo


Aidha, Mapunda ameipongeza Wilaya ya Kishapu kwa kuendeleza maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwainua mabinti na vijana waliokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali. Pia amepongeza ushirikiano na mawasiliano mazuri kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri, hasa katika kuwashirikisha wananchi katika miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa IPOSA.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Profesa Philipo Sanga, amewataka wanafunzi wanaonufaika na mradi huo kujituma katika masomo yao ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea maishani.


"Serikali inampango mzuri na kila mwananchi ndio maana hata sasa hakuna mwananchi asiyefikiwa na huduma zinazoletwa na serikali lengo lake kuu ni kuona kila mtu anauwezo wa kujisimamia kiuchumi licha ya kuwepo kwa tofauti ya majukumu" ameongeza SangaMwakilishi wa Kamishina wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST), Felister Mapunda, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya jengo la mradi wa Iposa lenye thamani ya Tsh. milioni 57.9 unaofadhiliwa na KOICA kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga  Machi 13,2026 ulioko Kijiji cha Negezi Kata ya Ukenyenge wilayani humo


Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa ambaye pia ni Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Mkoa wa Shinyanga, Dedan Rutazika, amewahimiza wanafunzi kuwa mabalozi kwa vijana wengine kwa kuwaelimisha kuachana na vitendo visivyofaa na badala yake kujikita katika kujipatia ujuzi wa fani mbalimbali kama ushonaji na mekanika.


Akizungumza kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mkurugenzi Mtendaji Emmanuel Johnson ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake mzuri na Serikali ya Korea uliowezesha kuletwa kwa mradi huo muhimu wilayani humo.Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa ambaye pia ni Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Mkoa wa Shinyanga, Dedan Rutazika, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya jengo la mradi wa Iposa lenye thamani ya Tsh. milioni 57.9 unaofadhiliwa na KOICA Machi 13,2026 ulioko Kijiji cha Negezi Kata ya Ukenyenge Wilayani Kishapu mkoani humo


Amesema mradi huo unaleta matumaini mapya kwa vijana waliokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali, na ameahidi kuwa halmashauri itausimamia kwa karibu ili kuhakikisha unaleta manufaa yaliyokusudiwa.


“Asanteni sana kwa kuchagua Kishapu. Nawapongeza pia wanafunzi wa IPOSA mlioamua kujiunga na mafunzo haya. Nawahakikishia kuwa ofisi ya Mkurugenzi iko tayari kuwasaidia na kutatua changamoto zozote mtakazokutana nazo kwa haraka na ufanisi,” amesema Johnson.


Mradi wa IPOSA unalenga kuwapatia ujuzi wa ufundi vijana wa kike na wa kiume waliokatisha masomo yao kwa sababu mbalimbali kupitia mafunzo ya fani za ushonaji na mekanika. Hadi sasa jumla ya wanafunzi 126 wamejisajili kuanza mafunzo katika kituo hicho.


Katika kuunga mkono juhudi hizo, Mkurugenzi Johnson pia ameahidi kutoa viti 100 vya ofisini ili kusaidia uendeshaji wa shughuli za mafunzo katika kituo hicho.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani shinyanga Emmanuel Johnson, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya jengo la mradi wa Iposa lenye thamani ya Tsh. milioni 57.9 unaofadhiliwa na KOICA na Halmashauri hiyo Machi 13,2026 ulioko Kijiji cha Negezi Kata ya Ukenyenge Wilayani Kishapu mkoani humoMratibu na Mfuatiliaji mradi wa IPOSA  Kyechun Lee akizungumzaNaibu Mhadhiri taalum na Mratibu wa IPOSA nchini Tanzania akizungumza Prof. Sempeho SiafuAfisa mfuatiliaji wa Mradi wa IPOSA nchini Tanzania Soobyn Au Diwani wa Viti maalumu wa Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephine MalimaMtaalamu wa elimu katika mradi wa IPOSA Efratha Kristos akizungumzaMkuu wa Divisheni ya Elimu ya awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Severine MsyangiAfisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Baraka Mwijarubi








































































































Post a Comment

0 Comments