Advertisement

Majina Waliochaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo vya kati 2025/2026 Yatangazwa!

 



Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imekamilisha mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati kwa mwaka wa masomo 2025.

 Orodha rasmi ya wanafunzi waliochaguliwa imewekwa wazi leo, [tarehe 06/06/2025], na inapatikana kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI www.tamisemi.go.tz

Wanafunzi wote wanaohusika na wazazi wanashauriwa kutembelea tovuti hiyo ili kupata Orodha ya Majina hayo.


KUANGALIA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KWENDA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA  KATI 2025/2026    👉👉👉👉 >>BOFYA HAPA ANGALIA


Idadi ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025


Kwa mujibu wa Waziri Mchengerwa, jumla ya wanafunzi 149,818, sawa na asilimia 69.96, wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano kwa mwaka huu wa masomo wa 2025/2026.


Hii ni hatua kubwa inayoonesha juhudi za serikali katika kuhakikisha vijana wanapata nafasi ya kuendelea na elimu ya juu ya sekondari.


Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo vya Ufundi na Ualimu

Mbali na kidato cha tano, serikali pia imetangaza majina ya wanafunzi 64,323 waliopata nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na ualimu, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kukuza ujuzi na maarifa ya vitendo kwa vijana wa Kitanzania.


Hii inalenga kuandaa nguvu kazi yenye weledi na uwezo wa kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa.


Waliokuwa na Sifa za Kuchaguliwa: Takwimu Muhimu


Katika mchakato mzima wa uchaguzi, wanafunzi 214,141 walibainika kuwa na sifa stahiki za kujiunga na elimu ya sekondari ya juu na vyuo vya ufundi.


 Kati yao, wasichana ni 97,517 huku wavulana wakiwa 116,624, jambo linaloonesha juhudi za serikali katika kutoa nafasi sawa kwa wote. 


Aidha, wanafunzi 1,028 wenye mahitaji maalumu pia walihusishwa katika mchakato huo, wakipata nafasi kama wengine ili kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma katika safari ya elimu.

Post a Comment

0 Comments